KOMBE LA SHIRIKISHO
Ratiba
**Mechi zote kuanza Saa 10 Jioni
Azam FC v Tanzania Prisons (Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam)
Yanga v Ndanda FC (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)
Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) litaendelea kwa michezo miwili ya Robo Fainali. 
Azam FC watakuwa kwenye uwanja wao wa Azam Complex huko Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kuwakaribisha Tanzania Prisons.
Nao Yanga watakuwa wenyeji wa Ndanda FC katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Robo Fainali za Kombe hili itakamilika Aprili 11 wakati Simba SC watakapocheza na Coastal Union katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Mwadui FC ndio timu pekee mpaka sasa ambayo imeshafuzu hatua ya Nusu Fainali, baada ya kuwachapa Geita Gold kwa mabao 3 -0.
Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) atawakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.
KOMBE LA SHIRIKISHO
Ratiba
Jumatatu Aprili 11
Simba v Coastal Union ( Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment