Wajasiriamali wanufaika mikopo ya Sh. bilioni 21

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Ibrahim Mwangalaba, wakati hafla ya kuorodheshwa hisa zao katika Soko la Hisa Dar es Salaam Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mipango, Fedha na Uchumi wa benki hiyo, Ashitu Mukangala, alisema wamefanikiwa kutoa mikopo hiyo kwa wajasiriamali kwa ununuzi wa bei nafuu ya hisa, jambo ambalo limewafanya wanufaike na mikopo ikiwamo kusaidia benki hiyo kupata faida ambayo inachangia kwa jamii kupata mikopo.
Mukangala alisema mikopo hiyo ambayo imetolewa mwaka jana, imeleta changamoto kwa wajasiriamali kujitokeza kujiunga na benki hiyo kama moja ya mkombozi kwa wananchi.
Alisema tukio la kuodhozeshwa hisa zao katika Soko la Hisa, kutaifanya benki hiyo ijitanue zaidi katika utoaji huduma kwa jamii nchi nzima.
"Tumefurahi kuona tunapiga hatua katika kuinua maendeleo ya jamii. Tulianza na mtaji wa Sh. bilioni 4.5, sasa umefikia Sh. bilioni 7.3," alisema Mukangala.
Naye Naibu Waziri Fedha na Mipango, Ashatu Kijazi, alisema amefurahishwa na changamoto kubwa za maendeleo zinazoonyeshwa na benki hiyo na kwamba anaamini watafika mbali katika kuhakikisha wanamuinua kila Mtanzania.
Alisema ofisi yake itakuwa mstari wa mbele kuzifanyia kazi changamoto wanazokabiliana nazo kwa sababu lengo ni kuona wazawa wananufaika na nchi yao katika upanuaji wa maendeleo.

0 comments:
Post a Comment