ANGA MDOMONI MWA TIMU KUTOKA ANGOLA KTK CAF


Baada ya Yanga kufungwa mabao 2-1 na Al Ahly ya Misri na hivyo kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2, timu hiyo ya Jangwani sasa imepangiwa timu kutoka Angola katika Kombe la Shirikisho hatua ya mtoano.

Kanuni za Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) zinaeleza kuwa timu ambazo zitatolewa katika Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika zitashuka katika Kombe la Shirikisho ambapo huko zitakutana na timu nane zilizosonga mbele ambapo zitacheza mechi za mtoano za nyumbani na ugenini kisha zitakazofuzu zitaingia hatua ya makundi.

Baada ya Yanga kutolewa, sasa itakutana na Sagrada Esperança baada ya droo kupangwa jana huku Yanga ikitakiwa kuanzia nyumbani wiki ya Mei 6-8, mwaka huu na marudio ni Mei 17-18, 2016.

RATIBA KAMILI YA MTOANO KOMBE LA SHIRIKISHO IPO HIVI: 


MO Béjaïa (Algeria)     Vs     (Tunisia) Espérance de Tunis Stade Malien (Mali)    Vs        (Morocco) FUS Rabat
Étoile du Sahel (Tunisia)     Vs    (Gabon) CF Mounana
TP Mazembe (DR Congo)     Vs    (Tunisia) Stade Gabèsien 
Al-Ahli Tripoli (Libya) Vs         (Misri) Misr El-Makasa
Al-Merrikh (Sudan)     Vs    (Morocco) Kawkab Marrakech 
Young Africans (Tanzania)     Vs    (Angola) Sagrada Esperança 
Mamelodi Sundowns (Sauz) Vs     (Ghana) Medeama 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment