
Gareth Bale amefunga magoli mawili kuisaidia Real Madrid kutoka nyuma kwa magoli mawili na kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya majirani zao Rayo Vallecano kuendeleza ndoto za kufukuzia ubingwa wa La Liga.
Vallecano walianza kuonza kwa magoli 2-0 ndani ya dakika 14 kwa magoli yaliyofungwa na Adri Embarba pamoja na Miku.
Bale aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Toni Kroos lakini kwa mara nyingine tena Real ilimpoteza Karim Benzema aliyepata majeraha.
Lucas Vazquez aliyeingia kuchukua nafasi ya Benzema, aliifungia Madrid bao la kusawazisha kabla ya Bale kuipa Madrid pointi tatu kwa goli lake la dakika za majeruhi.
Kikosi cha Zidane kilimkosa nyota wake Cristiano Ronaldo mbaye bado hakuna hakika kama atasafiri na timu kwenda kuikabili Manchester City baada ya kupata maumivu ya nyama za paja kwenye mchezo wa ligi siku ya Jumatano walipoibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Villarreal.
Maneja huyo wa Real aliwapumzisha Sergio Ramos pamoja na kiungo Casemiro na Luka Modric akijiandaa kuikabili Manchester City kwenye mchezo wa klbau bingwa Ulaya.

0 comments:
Post a Comment