JACK WILSHERE ATEMBELEA KICHAPO USIKU WA MANANE WENGER AMWAZIA


ARSENAL-WILSHIRE-ZOEZI
Jack Wilshere huenda akalikwaa rungu la Meneja wa Arsenal Arsene Wenger baada kubambwa kwenye ngumi za Mtaani Saa 8 za Usiku zilizotokea Jumamosi kuamkia Jumapili
 nje ya Kiota cha Usiku huko Jijini London kiitwacho Cafe de Paris.
 
Tukio hilo liko mikononi mwa Polisi ambao wamesema hakukamatwa Mtu ila uchunguzi wao unaendelea.

Wilshere, ambae amerejea Mazoezini Wiki iliyopita baada ya kuwa nje ya Uwanja tangu Agosti akiuguza Mguu wake uliovunjika, amekanusha kuhusika na ugomvi huo.
Hata hivyo, Maafisa wa Arsenal wametoboa Mchezaji huyo wa Timu ya Taifa ya England ataitwa Ofisini kwa Wenger Jumatatu wakati Timu itakapokusanyika Mazoezini kwenye Kituo chao cha Colney.

JACK WILSHERE – Historia ya rabsha zake:
-2010 Alikamatwa kwa ugomvi nje ya Naitiklabu na baadae kuonywa.
-2011 Akiri kosa na kuonywa na Polisi baada ya kujaribu kumtemea mate Dereva wa Teksi alievaa Kofia ya Mahasimu wa Arsenal, Tottenham Hotspur.
-2012 Aonywa na UEFA baada kuposti kwenye Mtandao wa Twitter kuhusu kucheza Kamari wakati wa Mechi ya Arsenal ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
-2013 Afungiwa Gemu 2 kwa kutoa ishara ya Matusi kwa Mashabiki wa Manchester City.
-2013 Abambwa nje ya Naitiklabu Jijini London akishika Sigara.
-2014 Sky Sports yaomba radhi baada kurusha matangazo aliyosikika Wilshere akiimba Matusi dhidi ya Tottenham wakati wa Paredi ya Arsenal Mitaani kutembeza FA Cup walilolibeba.
-2014 Anaswa akivuta Sigara kwenye Bwawa la Kuogelea huko Las Vegas, USA wakati wa Pati mara tu baada ya England kutupwa nje ya Kombe la Dunia huko Brazil.
-2015 Anaswa akishika Mtemba wa Shisha ndani ya Naitiklabu Jijini London.
-2015 Aomba radhi kwa kunaswa tena akiitukana tena Tottenham wakati wa Paredi ya Arsenal Mitaani kutembeza FA Cup walilolibeba kwa mara ya pili.
+++++++++++++++++++++++++++
Shahidi mmoja wa tukio hili la sasa, ambalo lilitokea takriban Saa 8 na Robo Usiku, amedai Wilshere, alieonekana kuwa mitungi, alizozana na kundi jingine la Watu huku akisaidiwa na wenzake na alipoona anapigwa Picha akafunika Uso wake.
Lakini kabla mambo hayajaharibika, Polisi wakawasili na kutenganisha Makundi hayo mawili yaliyokuwa yakizozana.
Wilshere amekataa katakata kuhusika na ugomvi na mmoja wa Marafiki zake amesistiza Mchezaji huyo hakurusha ngumi ingawa Polisi wameeleza yupo Mtu alielalamika kupigwa.
Kwa sasa Klabu ya Arsenal imedai tukio hilo ni ishu ya kibinafsi na itashughulikiwa ndani ya Klabu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment