
Kama utakuwa ni mpenzi wa kufuatilia stori za entertaiment basi hizi hapa zisikupite,millardayo.com imekurekodia stori zote za April 21 2016 ambazo zimepata airtime kupitia 255 ya XXL na hii ni moja kati ya stori ambayo imepata airtime, stori hii inamhusu Joh Makini na video yake mpya.
Joh Makini ana mpango wa kusafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kufanya video yake nyingine lakini mpaka sasa hajui ni wimbo gani anaenda kuufanyia video……
>>>’Natarajia kufanya vitu vingine vikubwa kwenye huu muziki tofauti na ambavyo umeshavisikia, ninaweza nikasafiri mwisho wa hii wiki kwa ajili ya kwenda kufanya video lakini mpaka sasa sijajua ni wimbo gani naenda kufanyia, muda huu tunaenda wote mimi, Nikki II na G Nako lakini kila mmoja ana project yake‘:-Joh Makini

Joh Makini

0 comments:
Post a Comment