KIJANA WA UMRI WA MIAKA KUMI NA SABA AWASHUSHA DARAJA ASTON VILLA





Aston Villa wameshushwa Daraja kutoka Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza toka 1987 baada ya kufungwa 1-0 na Manchester United Uwanjani Old Trafford hii Leo.

BPL-APR16A
Bao pekee lilifungwa na Chipukizi Marcus Rashford baada kupokea Pasi kutoka kwa Antonio Valencia ambae nae alikontroli vizuri pande refu toka kwa Kepteni Wayne Rooney alieanza Mechi yake ya kwanza tu baada ya kuwa nje kwa Miezi Miwili akijiuguza Goti.
Bao hilo ni la 7 kwa Rashford katika Mechi 12 alizoichezea Man United Msimu huu.
Kwa Aston Villa hiki ni kipigo chao cha 9 mfululizo kilichohakikisha wanashuka Daraja kwa mara ya 5 katika Historia yao.
VIKOSI:
Manchester United: De Gea, Valencia, Smalling, Blind, Rojo, Schneiderlin, Fellaini, Mata [Fosu-Mensah, 90’], Rooney [Lingard, 67’], Memphis, Rashford [Martial, 76’]
Akiba: Romero, Darmian, Fosi-Mensah, McNair, Young, Lingard, Martial
Aston Villa: Guzan; Hutton, Clark, Lescott, Cissokho, Bacuna, Westwood, Gana, Richardson [Gestede, 82’], Sinclair, Ayew
Akiba: Bunn, Richards, Sanchez, Gilm Lyden, Gestede, Grealish
         
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment