KLABU YA TOTTENHAM YAPATA PIGO LINGINE.

KIUNGO wa Tottenham Hotspur, Dele Alli, amefungiwa Mechi 3 na FA, Chama cha Soka England kwa kosa la Uchezaji wa Fujo.
Alli alinaswa kwenye TV akimpiga ngumi Mchezaji wa West Bromwich Albion wakati wa Mechi yao ya Ligi Jumatatu Usiku walipotoka Sare 1-1 Uwanjani White Hart Lane na kufunguliwa Mashitaka na mwenyewe kukiri kosa lake.
Alli, mwenye Miaka 20, Jumapili iliyopita alishinda Tuzo ya PFA, Professional Footballers Association, Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa, ya Mchezaji Bora wa Mwaka Kijana huko England.
Tukio hilo halikuwemo kwenye Ripoti ya Refa lakini kwa vile limenaswa kwenye TV FA wamepaswa kulipeleka kwenye Jopo maalum la Marefa Watatu Wastaafu ambao hulipitia na wakiafiki kuwa endapo Refa wa Mechi angeliliona basi angepaswa kutoa Kadi Nyekundu FA wanawajibika kumfungulia Mashitaka Mchezaji anaehusika na hilo ndio likafanyika na Alli kukiri kosa ingawa alihoji kufungiwa Mechi 3 ni Adhabu kubwa.
Kifungo hiki cha Alli cha Mechi 3 kinamaanisha atazikosa Mechi zote 3 za Spurs za Ligi zilizosalia Msimu huu.

MECHI za mwisho:
**h=Nyumbani
**a=Ugenini
Leicester City
Tottenham Hotspur
Jumapili 1 MeiMan United (a)
Jumatatu 2 MeiChelsea (a)
Jumamosi 7 MeiEverton (h)
Jumapili 8 MeiSouthampton (h)
Jumapili 15 MeiChelsea (a)
Jumapili 15 MeiNewcastle (a)

Adhabu hii kwa Alli imekuwa pigo kubwa kwa Spurs kwani amekuwa Kiungo muhimu kwao Msimu huu kwa kuiendesha Timu Uwanjani na yeye mwenyewe kufunga Bao 10.
Hivi sasa, Spurs wapo Nafasi ya Pili Pointi 7 nyuma ya Vinara wa Ligi Leicester City Gemu zikiwa zimebaki 3 tu.
Leicester wanaweza kutwaa Ubingwa Mechi yao ijayo Jumapili ikiwa wataifunga Manchester United Jumapili huko Old Trafford.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment