

Manchester United Leo walinaswa wakifanya Mazoezi yao ya mwisho kwenye Kambi yao ya Mazoezi ya AON Complex huko Carrington Jijini Manchester kabla kusafiri kwenda London kwa ajili ya Nusu Fainali ya FA CUP na Everton.
Jana, Meneja wa Man United, Louis van Gaal, alitoboa kuwa Timu haina Majeruhi yeyote baada ya Mechi ya Jumatano Uwani Old Trafford walipoifunga Crystal Palace 2-0.
Wasiwasi ulikuwa kwa Straika Chipukizi, Marcus Rashford, amabe alitolewa Kipindi cha Pili kwenye Mechi na Palace baada ya kuumizwa na ngwala ya Beki wa PalaceAdrian Mariappa lakini Kijana huyo wa Miaka 18 Leo alionekana akipiga tizi kwa furaha pamoja na Chipukizi mwenzake Timothy Fosu-Mensah na kina Marouane Fellaini na Jesse Lingard.
wanaweza kupona na kurejea Kikosini.
Njia kufika Nusu Fainali:

-Man United:
-Raundi ya 3, 1-0 v Sheffield United
-Raundi ya 4 3-1 v Derby County (A)
-Raundi ya 5 3-0 v Shrewsbury Town
-Raundi ya, 1-1 v West Ham United (Old Trafford); Mzarudiano, 2-1 v West Ham United (Upton Park).
-Everton:
-Raundi ya 3, 2-0 v Dagenham & Redbridge
-Raundi ya 4, 3-0 v Carlisle United;
Raundi ya 5, 2-0 v AFC Bournemouth;
-Raundi ya 6, 2-0 v Chelsea.
FA CUP
Ratiba
**Mechi zote kuchezwa Uwanja wa Wembley Jijini London
**Saa za Bongo
Jumamosi Aprili 23
1915 Everton v Manchester United
Jumapili Aprili 24
1800 Crystal Palace v Watford United

0 comments:
Post a Comment