MESS LEO PATASHIKA HAMWOGOPI MTU.

MESSI-SHANGILIA-BARCAMechi za Marudiano za Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI zinaanza Jumanne Usiku na Jumatano Usiku ipo mitanange miwili huko Jijini Madrid na Lisbon wakati Atletico Madrid itakapocheza na Mabingwa Watetezi FC Barcelona na Benfica kuikaribisha Bayern Munich.
Wageni wa Mechi 
hizi za Jumatano, Barca na Bayern, wote watatinga wakiwa na ushindi wa Nyumbani kwao wa Wiki iliyopita ambapo Barca iliichapa Atletico 2-1 na Bayern kuifunga Benfica 1-0.
Licha ya kushinda Mechi ya Kwanza, Barca wanatinga Vicente Calderon kuwavaa Atletico wakiwa hawajashinda Mechi 3 za La Liga lakini Supastaa wao, Lionel Messi, ambae ndie Mchezaji Bora Duniani kwa sasa, amesisitiza wao wanajiamini na wana nia ya kutinga Nusi Fainali UCL.
Kwenye La Liga, Barca walianza kwa Sare na Villareal na kisha kufungwa na Real Madrid na kisha Real Sociedad na kuufanya uongozi wao wa La Liga toka kwa Timu ya Pili Atletico kupungua na kuwa Pointi 3 tu.
Atletico ndio kikwazo cha Barca kutetea Taji lao la Ulaya lakini Messi amesisitiza: “Akili zetu ni zile zile tu. Tunahangaika Mwaka mzima ili kubeba Mataji mwishoni mwa Msimu. Tunajiamini wenyewe!”
Barca bado wako kwenye vinyang’anyiro vya kutwaa Trebo Msimu huu kama ilivyokuwa Msimu uliopita walipotwaa Ubingwa wa La Liga, UCL na Copa del Rey ambayo wako Fainali na watacheza na Sevilla Mwezi ujao.
ROBO FAINALI
Marudiano
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
**Mechi kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku
Jumanne Aprili 12
Manchester City v Paris St-Germain [2-2]
Real Madrid v Wolfsburg [0-2]
++++++++++++++++++++++++++++++
TAREHE MUHIMU:
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment