Sido yatoa mikopo zaidi ya Sh milioni 505

SHIRIKA la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (Sido) mkoani Singida limetoa mikopo kwa wanufaika mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 505, kati ya Januari Mosi na Desemba 31 mwaka jana.
Ofisa Mikopo wa Sido mkoani Singida, Reuben Mwanja alisema mjini hapa juzi kuwa walengwa 1,089 walionufaika na mikopo hiyo na kati yao, 675 ni wanawake na 414 ni wanaume.
Mwanja alisema mikopo ya Sh milioni 354.8 ilitolewa kupitia wateja 774 wa vikundi; wanawake wakiwa 509 na wanaume 265 wakati Sh milioni 150.7 zilitolewa kwa mteja mmoja mmoja.
Kwa mujibu wa Mwanja vikundi vingi vya vijijini vilivyopewa mikopo hiyo, ni vilivyopo kwenye utaratibu wa Vicoba, ambavyo ni Mhintiri, Igombwe na Ikungi vyote vya Wilaya ya Ikungi “Marejesho ya mikopo hii ni asilimia 98 hali inayoridhisha mno,” alisema Mwanja.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment