
Barcelona imeendelea kukaa kileleni mwa La Liga ikizipiku Atletico Madrid na Real Madrid zinazomfutia kwa karibu baada ya kuichakaza Sporting kwa magoli 6-0.
Kutoka kwenye majanga ya vipigo, Barcelona imekuja na moto mkali kwa ushindi mkubwa kwenye mechi mbili mfululizo wakianza na ule wa bao 8-0 dhidi ya Diportivo kabla ya ushindi wa Jumamosi usiku.

Licha ya kupata ushindi wa magoli ya kujaza kapu, Barca bado inakabiliwa na upinzani mkubwa licha ya kuwa na faida ya matokeo ya head-to-head endapo kama ligi itamalizika huku kukiwa na kulingana kwa pointi dhidi ya timu zinazowania ubingwa wa La Liga.
Messi alianza kuzifungua kamba za Sporting Gijon mapema kipindi cha kwanza akifunga bao moja pekee kati ya mabao sita yaliyofungwa kwenye mchezo huo.

Baadaye Suarez alipachika bao la pili na matokeo kuwa 2-0. Penati mbili za harakaharaka zilizofungwa na Suarez zikafanya matokeo kuwa 4-0.
Dakika tano kabla ya mchezo kumalizika ikapatikana penati nyingine ambayo ilifunwa na Neymar na kuifanya safu ya ushambuliaji ya Barca (MSN) kila mmoja kufunga bao kwenye mchezo huo
Suarez akapiga bao lake la nne kwenye mchezo huo dakika za lala salama na kukamilisha ushindi wa Barcelona 6-0 Sporting Gijon.

Zikiwa zimesalia game tatu, Barcelona inaongoza ligi kwa pointi 82 sawa na Atletico Madrid huku Real Madrid ikifuatia kwa pointi zake 81.

0 comments:
Post a Comment