Watu 60 wafariki kutokana na mafuriko Pakistan



Watu 60 wamefariki kutokana na mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha maeneo ya kaskazini magharibi mwa Pakistan, maafisa wanasema.
Mvua kubwa ilianza kunyesha Jumamosi na kusababisha mafuruiko mikoa ya Khyber Pakhtunkhwa, Kashmir na Gilgit Baltistan.
Ingawa msimu wa mvua za pepo za msimu haujaanza, mvua za kabla ya msimu mara nyingi husababisha uharibifu hasa maeneo ya mashambani Pakistan ambapo miundo mbinu ni duni.

MvuaImage copyrightGetty
Image captionMaeneo ya mashambani ndiyo yaliyoathirika zaidi

Maafisa wamesema wakazi wametakiwa waondoke na kukimbilia nyanda za juu na maeneo yaliyo salama.
Mwaka uliopita, zaidi ya watu 170 waliuawa wakati wa msimu wa mvua za masika nchini Pakistan.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment