BURUDANI EXCLUSIVE: Lulu kaongea kwanini Kanumba day hakwenda kwenye kaburi la Kanumba wala kumpost

Maswali yalikua ni mengi na mashabiki walitaka kufahamu kwanini mwigizaji Lulu kutoka kwenye kiwanda cha filamu Tanzania hakumpost kwenye Instagram kama ishara ya kuonyesha ulimwengu kwamba anamkumbuka Marehemu Steven Kanumba na vilevile hakuhudhuria kwenye kaburi la Kanumba kama walivyofanya wengine.
Siku hiyo ya kutimia kwa miaka minne ya kifo cha Kanumba (Kanumba Day), Waigizaji mbalimbali wa movie Tanzania pamoja na watu wengine kama Mama Kanumba pamoja na Mama Lulu walikwenda kaburini lakini Lulu hakuonekana.
Kuhusu kutokuonekana kwake Lulu kwenye Exclusive DIMBA.com ameongea kama ifuatavyo >>> ‘Kiukweli sikuwahi kutaka kuongelea chochote kuhusu hiki kitu kwasababu ninachoamini mimi nina maumivu kuliko mtu yeyote anaedhani nina maumivu, ile siku ni maalum kwa taifa au kwa watu wengine lakini kwangu Kanumba Day ni kila siku
Kama watu walikwenda siku ile mimi naweza nikaenda leo, nikaenda kesho… tatizo watu wengi wako-fake wanataka kuonekana wamefanya, mimi naweza kufanya kitu na mtu yeyote asijue nimefanya, sidhani kama kumuenzi mtu vinatakiwa kuanza kutangazwa… hii sio biashara kama natafuta Wateja, najua kiimani kidini unatakiwa kufanya vitu gani kumuenzi mtu.. hivyo ndivyo ninavyofanya mimi‘ – Lulu
KUHUSU MAMA KANUMBA: ‘Kuhusu Mama Kanumba sitotaka kuzungumzia chochote kuhusu yeye kwa sababu naamini kama iko siku itanilazimu kuongea sanaa nitaongea’
UNATAKA KUMSIKILIZA LULU ZAIDI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment