KIUNGO wa France Lassana Diarra ameamriwa kulipa Faini ya Euro Milioni 10 kwa Klabu yake ya zamani Lokomotiv Moscow.
Amri hiyo imetolewa na Mahakama ya Usuluhishi Michezoni (CAS-Court
for Arbitration in Sports) baada ya Mchezaji huyo kutimka Klabu hiyo ya
Russia Mwaka 2014 Mshahara wake ulipopunguzwa.
Diarra, mwenye Miaka 31 na ambae alicheza England akiwa na Chelsea
na kutwaa FA CUP Mwaka 2007 na pia kubeba tena Kombe hilo Mwaka
uliofuata akiwa na Portsmouth, sasa anachezea Marseille ya France.
Pia Kiungo huyo ni mmoja wa Kikosi cha Wachezaji 23 wa France ambacho kitacheza EURO 2016 kuanzia Juni 10 Nchini humo France.
Diarra alikatisha Mkataba wake Mwaka mmoja tu baada ta kuwa nao
pale Mshahara wake ulipopunguzwa na kufungiwa Miezi 15 bila Mshahara na
baada ya hapo akajiunga na Marseille.
Akipokea hii adhabu yake mpya, Diarra aliandika kwenye Twitter:
"Yote ni kufungiwa Miezi 15, nimeshatumikia, kutolipwa Mishahara Miezi
15, nimetumikia, Euro 110,000 kwa CAS, zimelipwa na sasa Euro Milioni
10!"

0 comments:
Post a Comment