Dani Alves ajiunga na Messi na Figo katika listi ya watengeneza magoli bora wa muda wote wa La Liga

Beki wa kimataifa wa Brazil Dani Alves amekuwa nguzo muhimu katika mafanikio ya klabu ya FC Barcelona katika 10 iliyopita.
Mbrazil huyo ambaye ameshashinda ubingwa wa La Liga mara 6, jana ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa 3 katika historia ya ligi kufikisha assists 100 – akiungana na Luis Figo na Lionel Messi.
image
Mbrazil huyo alitengeneza goli la pili la Suarez katika mchezo dhidi ya Granada, mechi iliyoipa ubingwa Barcelona katika siku ya mwisho ya ligi.
Na assist aliyompa Suarez ikatimiza idadi ya 100 kwa Alves ambaye alianza kucheza La Liga tangu msimu wa 2003.
image
Lionel Messi ndio anaongoza kwa kutoa assist katika historia ya La Liga akiwa na assist 127, wakati Luis Figo katika misimu yake 10 ya La Liga akiwa na Barca na Real Madrid alifanikiwa kutimiza assist 105 – Alves anafuatia akiwa na assist 100, na huenda akampiku Figo kuanzia msimu ujao.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment