Sheffield
Wednesday wakiwa Uwanjani kwao imejiweka pazuri kutinga Fainali ya
Mechi za Mchujo kusaka Timu ya 3 iliyobakia kupanda Daraja kutoka
Championship kwenda BPL, Ligi Kuu England baada ya kuifunga Brighton Bao
2-0.
Wiki iliyopita, Middlesbrough iliungana na Burnley kupandishwa Daraja toka Championship kwend BPL, Ligi Kuu England na Nafasi ya 3 na ya mwisho kwa Timu kupanda BPL inapatikana baada ya Mechi za Mchujo zinazohusisha Timu zilizomaliza Nafasi za 3 hadi za 6.
Mechi hizo zinachezwa nje ndani na Washindi kutinga Fainali Wembley.
Usiku wa Leo Ijumaa, Bao za ushindi za Sheffield Wednesday zilifungwa na Ross Wallace Dakika ya 45 na Kieran Lee Dakika ya 73.

Ijumaa Derby County wataivaa Hull City katika Mechi nyingine ya Mchujo.
VIKOSI:
Sheffield Wednesday: Westwood; Hunt, Lees, Loovens, Pudil; Wallace, Lee, Lopez, Bannan; Hooper, Forestieri.
Akiba: Wildsmith, Hutchinso
n, Matias, Nuhiu, Helan, Joao, Sasso
Brighton: Stockdale; Bruno, Goldson, Greer, Bong; Knockaert, Sidwell, Kayal, Skalak; Baldock, Hemed.
Akiba: Maenpaa, Calderon, Rosenior, Towell, LuaLua, Murphy, Wilson.
REFA: Andre Marriner
CHAMPIONSHIP
Mechi za Mchujo
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Ijumaa Mei 13
Sheffield Wednesday 2 Brighton 0
Jumamosi Mei 14
1430 Derby Count v Hull City
Marudiano
Jumatatu Mei 16
2145 Brighton v Sheffield Wednesday [0-2]
Jumanne Mei 17
2145 Hull City v Derby County
Fainali
Wembley Stadium, London
Jumamosi Mei 28
**Saa 1900

0 comments:
Post a Comment