FA CUP 2016 -FAINALI KUZIKUTANISHA MAN U VS CYSTAL PALACE REFA ASHAJULIKANA TIKETI WAZI;

FACUP2016

FA, Chama cha Soka cha England, kimethibitisha Saa ya kuanza Mechi ya Fainali ya FA CUP ambalo kwa sababu za kiudhamini huitwa EMIRATES FA CUP.
Pia, FA imetangaza mgao wa Tiketi za Fainali hii kwa Klabu zitakazocheza, Crystal Palace na Manchester United.

Lakini kwa Mashabiki wengi wa Man United watakaotoka Jiji la Manchester wamekumbwa na wasiwasi mkubwa kuhusu kuwahi Treni ya mwisho baada ya Mechi hiyo.

Pambano hilo litaanza Saa 11 na Nusu Jioni, Saa za England, na endapo Mechi hiyo itakuwa Sare baada ya Dakika 90 basi zitapigwa Dakika za Nyongeza 30 na kisha, ikibidi, Mikwaju ya Penati Tano Tano.

Hilo litawawia vigumu Mashabiki wa Man United kuwahi Treni za mwisho 3 ambazo zitaondoka Saa 3 Usiku kwa Saa za huko.
Ili kupunguza adha hiyo Klabu ya Man United imepanga kuweka Mabasi maalum ya bure kuwasafirisha Mashabiki wenye Tiketi za Fainali hiyo.

Kila Klabu imepewa mgao wa Tiketi 28,780 ambazo Bei zake ni kuanzia Pauni 45, Shilingi 142,900, hadi Pauni 115, Shilingi 365,200.

Kwenye Fainali hiyo imeamuliwa Crystal Palace iwe Timu ya Nyumbani na hivyo kuvaa Jezi zao za kawaida Nyekundu na Bluu wakati Man United itahesabika kama Timu ya Ugenini na hivyo kuvaa Bukta Nyeusi na Shati Nyeupe.

Mbali ya kutwaa Kombe, Mshindi wa Fainali atazawadiwa Fedha Pauni Milioni 1.8 na Mshindi wa Pili Pauni 900,000.
Refa wa pambano hili ameteuliwa kuwa Mark Clattenburg.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment