Kwa mujibu wa BBC, fainali za michuano hiyo ya ulaya zitaoneshwa live kupitia mtandao wa YouTube.Warusha matangazo ya live ya mechi za ulaya, kampuni ya BT Sport ya Uingereza wataonesha mechi hizo kwenye channels zao na pia kwenye mtandao wa YouTube.
Kikosi
cha Jurgen Klopp cha Liverpool kitakutana na mabingwa watetezi Sevilla
katika fainali ya Europa, jumatano ya tarehe 18 May, wiki ijayo.Mahasimu wa La Liga Real Madrid na Atletico Madrid watafuatia kwa kukutana kwenye fainali ya mabingwa wa ulaya, Jumamosi ya tarehe 28 May.
Liverpool ambao mashabiki wao wengi watashindwa kusafiri kwenda Basel kushuhudia fainali, wameamua kuonyesha live mechi hiyo katika eneo la Echo Arena, ambalo lina uwezo wa kuingiza watu 9,000 waliokaa.
Mnamo
mwaka 2013, BT Sport walitangaza dili la miaka 3 lenye thamani ya £897m
kuonyesha mechi zote 350 za michuano hiyo ya Champions League na Europa
kuanzia mwaka 2015.Katika moja ya sehemu ya mkataba huo, BT ilisema kwamba itaonyesha bure japo mchezo mmoja ambao utahusisha timu kutoka England kwa kila msimu.

0 comments:
Post a Comment