Jan Oblak aifikia rekodi ya clean sheet iliyodumu kwa miaka 22

Golikipa wa Atletico Madrid ameweka rekodi mpya katika ligi kuu ya Hispania na kuifikia rekodi iliyodumu kwa miaka 22.
image
Jan Oblak ameifikia rekodi hiyo ya La Liga kwa kupata clean sheet nyingine katika mchezo wa kumaliza ligi dhidi ya Celta Vigo jana jumamosi.
Golikipa huyo wa timu ya taifa ya Slovenia amefanikiwa kutoruhusu nyavu zake kuguswa katika mechi 18 za ligi ya Hispania, idadi kubwa zaidi tangu golikipa wa Deportivo La Coruna Paco Liano alipofanikiwa na yeye kupata clean sheet 18 katika msimu wa 1993-94.
Oblak Amecheza mechi zote za msimu huu wa La Liga na kikoso cha Diego Simeone.
Pamoja na kuwa na rekodi nzuri ya ulinzi, lakini Atletico walishindwa kushinda ubingwa wa La Liga, badala yake wamemaliza nafasi ya 3 nyuma ya mabingwa FC Barcelona na washindi wa pili mahasimu wao Real Madrid.
Lakini kwa upande wa Oblak amefanikiwa kumaliza ligi akiwa golikipa bora wa La Liga huku akiongoza kwa kupata clean sheet nyingi pia katika michuano ya ulaya pia ambayo Atletico wanasubiri kucheza fainali wiki mbili zijazo jijini Milan.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment