Baada ya kumalizika kwa michezo ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kushuhudia klabu kutoka mji mmoja Real Madrid na Atletico Madrid zikifanikiwa kufika hatua ya fainali ya UEFA 2016, jina la refa atakayechezesha mchezo huo limetangazwa kuwa ni Mark Clattenburg kutoka Uingereza.
Mark Clattenburg
mwenye umri wa miaka 41 alitangazwa kuwa refa wa kimataifa toka mwaka
2007, lakini siku saba kabla ya kuchezesha mchezo huo wa fainali katika
jiji la Milan Italia, atachezesha mchezo wa fainali ya FA Cup Uingereza May 21 kati ya Man United dhidi ya Crystal Palace katika uwanja wa Wembley.
Clattenburg
ni moja kati ya marefa bora kwa sasa lakini aliwahi kufurahisha watu
pale alipoingia uwanjani akiwa kasahau kadi, wakati faulo inatokea
anaangalia mfukoni anajikuta hana kadi hadi alipoletewa.

0 comments:
Post a Comment