| WAWA |
Beki
wa kati wa Azam FC, Muaivory Coast, Pascal Wawa, amekiri kuwa katika
ligi ya msimu uliopita mambo yalimuendea kombo lakini amepiga mkwara
kuwa msimu ujao watamkoma kwa jinsi atakavyokuwa amejipanga.
Wawa
hakuweza kucheza mechi zilizobakia za Ligi Kuu Bara na za Kombe la
Shirikisho Afrika kufuatia kuuguza majeraha ya nyama za paja aliyoyapata
katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya
Esperance ya Tunisia uliopigwa jijini Dar.
Wawa
amesema kuwa licha ya kukosa ubingwa wa ligi kuu na Kombe la FA, lakini
anaamini hakuweza kucheza katika kiwango chake siku zote hali ambayo
hataki ijirudie msimu ujao.
“Ligi
imemalizika na Yanga imeonekana kuwa ni timu bora kwa kuweza kuchukua
makombe yote mawili lakini haikuwa rahisi kwao kwa sababu ushindani
ulikuwa mkubwa kwa kila timu ambayo unacheza nayo, ila bado naamini hata
sisi timu yetu ilikuwa bora, ingawa majeraha yameniangusha.
“Nadhani
kilikua kitu kibaya kwetu kuona tunashindwa kufikia malengo kwani
naamini msimu huu sikucheza katika kiwango changu, sijui kwa nini
imekuwa hivyo lakini sitarajii hali hii ijirudie msimu ujao, kwa sababu
narudi nyumbani kwa mapumziko halafu nitaenda Afrika Kusini kwa matibabu
zaidi na nikirejea msimu ujao nitakuwa tofauti zaidi,” alisema Wawa.
SOURCE: CHAMPIONI

0 comments:
Post a Comment