LEO HODGSON KUTAJA KIKOSI CHA ENGLAND EURO 2016, RASHFORD KUBAKI, STURRIDGE KUMWAGWA??

LEO Kocha wa England Roy Hodgson atatangaza rasmi Kikosi chake cha Wachezaji 23 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya EURO 2016 zinazoanza huko France hapo Juni 10.
Gumzo kubwa huko England ni kama Straika wa Liverpool Daniel Sturridge atabaki kwenye Timu na Chipukizi wa Manchester United Marcus Rashford kuwemo.
Sturridge amekuwa akiandamwa na maumivu ya mara kwa mara na hilo pia lilimfanya aikose Mechi ya Ijumaa England ilipoifunga Australia 2-1 huku Kinda Marcus Rashford akianza Mechi yake ya kwanza kabisa kwenye Kikosi cha England na kupiga Bao la Kwanza.
Lakini Jana Sturridge alijumuika na wenzake wa England Mazoezini wakiwepo Wachezaji wote wa 25 wa England waliobaki baada ya Kiungo wa Man City Fabian Delph kujiondoa Kikosini akijiuguza Nyonga.
Leo Hodgson anapaswa kupunguza Wachezaji Wawili ili awasilishe rasmi UEFA Wachezaji 23 kwa ajili ya EURO 2016.
Kama angekuwa fiti kwa Asilimia 100, kusingekuwa na mjadala kuhusu Sturridge kuwemo Kikosini lakini majeruhi ya mara kwa mara yamemfanya Straika huyo wa Liverpool aichezee England Dakika 58 tu tokea Septemba 2014.
Hilo limetoa mwanya mkubwa kwa Kinda wa Man United Marcus Rashford apate fursa ya kwenda France kwenye EURO 2016 hasa baada ya Ijumaa iliyopita ya kuwa Kijana mdogo kabisa kuifungia England Bao katika ya kwanza tu tangu 1938.
ENGLAND - KIKOSI CHA WACHEZAJI 25:
MAKIPA: Tom Heaton (Burnley), Fraser Forster (Southampton), Joe Hart (Manchester City)
MABEKI: Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Danny Rose (Tottenham Hotspur), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton), Kyle Walker (Tottenham Hotspur)
VIUNGO: Dele Alli (Tottenham Hotspur), Ross Barkley (Everton), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Danny Drinkwater (Leicester City), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City), Andros Townsend (Newcastle United). Jack Wilshere (Arsenal)
MAFOWADI: Harry Kane (Tottenham Hotspur), Daniel Sturridge (Liverpool), Jamie Vardy (Leicester City), Wayne Rooney (Manchester United), Marcus Rashford (Manchester United)
ENGLAND – Mechi zao:
Ratiba/Matokeo:
Mei 2016
Kirafiki      
Jumapili Mei 22
England 2 Turkey 1       
Ijumaa Mei 27
England 2 Australia 1      
Juni 2016
Alhamisi Juni 2
2145 England v Portugal
EURO 2016 Kundi B      
Jumamosi Juni 11
2200 England v Russia   
Alhamisi Juni 16
1600 England v Wales       
Jumatatu Juni 2
2200 Slovakia v England
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment