LEO MARA YA KWANZA MARCUS RASHFORD NDANI YA ENGLAND KUIVAA AUSTRALIA!

Manchester United team-mate Marcus Rashford is in line to make his début at the Stadium of Light

LEO Usiku huko Stadium of Light, Uwanja wa Klabu ya Sunderland, Chipukizi wa Manchester United Marcus Rashford anatarajiwa kuchezea Kikosi cha Kwanza cha England kwa mara ya kwanza.
Rashford alipata nafasi kibahati kuichezea Timu ya Kwanza ya Man United baada ya Kikosi hicho kupata Majeruhi kadhaa Miezi Mitatu iliyopita na kung’ara huku akipiga Bao kadhaa muhimu.
Chipukizi huyo ambae amechezea Timu za Vijana wa England ameitwa kwenye Kikosi cha Wachezaji 26 wa awali wa England kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Ulaya EURO 2016 zinazoanza Juni 10 huko France.
Lakini Mechi ya Leo kwa Rashford ni mtihani mkubwa kwani akicheza vizuri yeye anaweza kuwemo kwenye Kikosi cha mwisho cha England cha Wachezaji 23 ambacho kitawasilishwa UEFA Jumanne Mei 31.
Alipodadisiwa kuhusu Rashford, Meneja wa England Roy Hodgson ameeleza: “Mimi, Makocha, na Wachezaji wengine pamoja na Dunia yote ya Soka ya England itakuwa ikitazama. Wote tunajua Chipukizi huyu ni spesho, Je anaweza kuonyesha?”
Hodgson alidokeza kumuamini Rashford pale alipotamka: “Tunatambua spidi yake. Tunatambua kushambulia kwake. Tunatambua anavyozizunguka Difensi akiwa na Mpira au hana. Tizama alivyocheza Fainali ya FA CUP, anacheza kwa kuamini uwezo wake. Ana vipaji maalum ambavyo vitasaidia staili yetu ya uchezaji!”
ENGLAND
Ratiba
Mei 2016
Kirafiki      
Jumapili Mei 22
England 2 Turkey 1       
Ijumaa Mei 27
2145 England v Australia      
Juni 2016
Alhamisi Juni 2
2145 England v Portugal
EURO 2016 Kundi B      
Jumamosi Juni 11
2200 England v Russia   
Alhamisi Juni 16
1600 England v Wales       
Jumatatu Juni 2
2200 Slovakia v England
Manchester United’s Marcus Rashford here to stay, says Michael Carrick
 Read more
“I can’t alter the fact that playing him will create headlines and exceptional interest but I suppose that is part of him being an international footballer and there is nothing I have seen in his make-up so far, watching him at Manchester United and seeing him these few days in training, that leads me to believe that isn’t the case. But we’ll see.”
ENGLAND - KIKOSI CHA WACHEZAJI 26:
MAKIPA: Tom Heaton (Burnley), Fraser Forster (Southampton), Joe Hart (Manchester City)
MABEKI: Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Danny Rose (Tottenham Hotspur), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton), Kyle Walker (Tottenham Hotspur)
VIUNGO: Dele Alli (Tottenham Hotspur), Ross Barkley (Everton), Fabian Delph (Manchester City), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Danny Drinkwater (Leicester City), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City), Andros Townsend (Newcastle United). Jack Wilshere (Arsenal)
MAFOWADI: Harry Kane (Tottenham Hotspur), Daniel Sturridge (Liverpool), Jamie Vardy (Leicester City), Wayne Rooney (Manchester United), Marcus Rashford (Manchester United)
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment