UEFA CHAMPIONZ LIGI
Nusu Fainali
Mechi za Pili
Jumanne Mei 3
**Kwenye Mabano Jumla ya Magoli kwa Mechi Mbili
Bayern Munich 2 Atletico Madrid 1 [2-2, Atletico wasonga kwa Bao la Ugenini]
Jumatano Mei 4
**Saa 3 Dakika 45 Usiku
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
Real Madrid v Manchester City [0-0]
Real Madrid Leo inarudiana na Manchester City kwenye Nusu Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI Uwanjani Santiago Bernabeu Jijini Madrid Mchini Spain na habari njema kwao ni kupona kwa Staa wao Cristiano Ronaldo.
Kocha wa Real anaetoka France, Zinedine Zidane, amethibitisha kuwepo kwa Ronaldo ambae hajacheza Mechi 3 sasa akisumbuliwa na Musuli za Pajani.
Ronaldo aliikosa Mechi ya kwanza ya Timu hizi Wiki iliyopita huko Etihad waliyotoka 0-0.
Kuwepo kwa Ronaldo, aliefunga Bao 47 Msimu huu 16 zikiwa za UCL na kumfanya awe Mfungaji Bora, kunaipa Real nguvu kubwa kushinda Mechi hii na kutinga Fainali kucheza na Mahasimu wao wakubwa Atletico Madrid.
Ronaldo anahitaji Bao 1 tu kuikamata Rekodi yake mwenyewe ya UCL ya Bao 17 katika Msimu mmoja aliyoiweka 2013/14.
Pia Zinedine Zidane amethibitisha kutocheza kwa Karim Benzema na Kiungo wa Brazil Casemiro wote wakiwa ni Majeruhi.
Kwa upande wa Man City chini ya Kocha kutoka Chile, Manuel Pellegrini, aliewahi kuifundisha Real Mwaka 2009 na 2010, habari njema kwao ni kurejea dimbani kwa Kiungo wao mahiri kutoka Ivory Coast, Yaya Toure, ambae alizikosa Mechi 2 baada kuumia Goti.
Lakini City itawakosa Majeruhi David Silva na Pablo Zabaleta pamoja na Kiungo Samur Nasri ambae hakusajiliwa kwa ajili ya Mashindano haya.
Uso kwa Uso:
Real Madrid hawajafungwa katika Mechi 3 walizocheza na Man City kwa kushinda 3-2 huko Santiago Bernabeu na Sare 2 za 1-1 na 0-0 huko Manchester.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Real Madrid (Mfumo 4-3-3):
Navas,
Marcelo, Ramos, Pepe, Carvajal,
Jese, Modric, Kroos,
Ronaldo, Bale, Vazquez
Manchester City (Mfumo 4-2-3-1):
Hart,
Kolarov, Otamendi, Kompany, Sagna,
Fernandinho, Fernando,
Sterling, De Bruyne, Navas,
Aguero.
REFA: Davir Skomina [Slovenia]
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Fainali
Jumamosi Mei 28
**Saa 3 Dakika 45 Usiku
Atletico Madrid v Real Madrid/Manchester City


0 comments:
Post a Comment