Licha ya kuifunga 6-1 Majimaji FC Oct 31 2015, Simba imeshindwa kupata point tatu Songea leo May 11

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo May 11 2016 kwa klabu ya Majimaji FC ya Songea kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu wa 29 dhidi ya Simba katika uwanja wa Majimaji Songea, huu ni mchezo ambao Simba hawapewi nafasi kubwa ya kupata matokeo mazuri kutokana na baadhi ya wachezaji wake kutosafiri na timu.
Katika mchezo wa kwanza ambao Simba walicheza na Majimaji FC Dar es Salaam uwanja wa Taifa October 31 2015, Simba walionekana kuwa wababe wa Majimaji FC kwa kufunga jumla ya goli 6-1, huku Ibrahim Ajib akipiga hat-trick katika ushindi huo, takwimu hizo hazikuifanya Simba kupata matokeo katika uwanja wa Majimaji.
Wakiwa katika uwanja huo wa ugenini Simba wametoka sare ya 0-0, licha ya takwamu za mchezo wao wa awali dhidi ya Majimaji waliocheza uwanja wa Taifa Dar es Salaam waliibuka na ushindi wa goli 6-1. kufuatia matokeo hayo Simba sasa inaendelea kuwa nafasi ya tatu kwa kufikisha jumla ya point 59.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment