Michuano
ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) msimu wa 2015/2016 inaendelea vizuri
katika vituo vinne vya Kagera, Morogoro, Singida na Njombe ambapo
itafikia tamati Juni 6 mwaka huu.
Timu
sita zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa
2016/2017. Timu hizo ni zile zitakazoongoza kila kundi, na washindwa
bora (best losers) wawili kutoka makundi mawili tofauti.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeweka waangalizi wake katika kila
kituo, na litawachukulia hatua watu wote watakaobainika kutumia michuano
hiyo kuchafua viongozi.
Mtwivila
City ya Iringa inaongoza kituo cha Njombe ikiwa na pointi sita baada ya
kucheza mechi tatu. Katika kituo hicho kesho (Mei 31) kutakuwa na mechi
kati ya Jangwani FC ya Rukwa na Nyundo FC ya Katavi kwenye Uwanja wa
Amani.
Timu
inayoongoza kituo cha Morogoro ni Namungo FC ya Lindi yenye pointi saba
kwa mechi tatu. Kesho (Mei 31) ni mechi kati ya Makumbusho FC na
Sifapolitan, zote za Dar es Salaam itakayofanyika Uwanja wa Jamhuri
mjini Morogoro.
Kitayose
ya Kilimanjaro inaongoza kituo cha Singida ikiwa na pointi tisa baada
ya kushinda mechi zote tatu ilizocheza. Kesho (Mei 31) kwenye kituo
hicho kutakuwa na mechi kati ya Stand FC ya Tabora na Murusgamba ya
Kagera itakayochezwa Uwanja wa Namfua.
Mpaka
sasa vinara wa Kituo cha Kagera ambacho mechi zake zinachezwa Uwanja wa
Vijana mjini Muleba ni Mashujaa FC ya Kigoma yenye pointi saba.


0 comments:
Post a Comment