List ya makocha Uingereza kufukuzwa imeongeza, mwingine kapoteza ajira yake leo May 12 2016

Headlines za makocha wa soka kupoteza ajira zao zinazidi kugonga vichwa vya habari kila kukicha duniani kote, Alhamisi ya May 12 2016 jina la kocha Roberto Martinez limeingia kwenye list ya makocha waliofukuzwa Ligi Kuu Uingereza msimu huu wa 2015/2016.
Baada ya kupokea vipigo, klabu ya Everton imetangaza kumfukuza kazi kocha wake Roberto Martinez, Everton hivi karibuni kabla ya mchezo wa jana usiku kukubali kipigo cha goli 3-0 kutoka kwa Sunderland, katika michezo yake mitano iliyopita ilikuwa imefungwa mechi tatu, sare mechi moja na ushindi mechi moja.
_89629591_roberto_martinez_pa
Roberto Martinez
Kwa sasa Everton ambayo imebakiza mechi moja ili kumaliza msimu wa Ligi Kuu Uingereza, ipo nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi, imecheza mechi 37, ina point 44, imefungwa mechi 13, imeshinda mechi 10 na kutoa sare mechi 14, hii ni kwa mujibu wa Sky Sports na BBC.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment