Matokeo
yake, wawekezaji ambao waliwekeza kwenye soka katika kipindi cha mika
10 iliyopita sasa wanavuna mapato makubwa hasa katika timu za England.UEFA imeongeza malipo katika Champions League kwa asilimia 50% kwa miaka 3 kuanzia msimu wa 2015-16. Fainali ya mwaka huu, itakayochezwa San Siro jijini Milan, Italy, baina ya vilabu vya Spain, Real Madrid vs Atletico, kila timu itapata kiasi cha $100 million.

Vilabu 20 ambavyo vinaongoza kwa uthamani vina thamani ya wastani wa $1.44 billion, ongezeko la 24% kuliko ilivyokuwa miaka 20 iliyopita. Malipo makubwa ya dili za TV, kama mkataba wa miaka wa miaka 3 wenye thamani ya $7.9 billion baina ya English Premier Keague na Sky Sports na BTSport ambao unaanza msimu wa 2016/17, na dili nyingine za udhamini wa jezi, mfano ukiwa mkataba wenye thamani ya $130m kwa mwaka baina ya Manchester United na Adidas.
Timu
yenye thamani kubwa ya soka kwa mwaka wa nne mfululizo ni Real Madrid
wakiwa na thamani ya $3.65 billion, ongezeko la 12% la thamani
waliyokuwa nayo mwaka uliopita.
Wanaowafuatia ni FC Barcelona ambao wana thamani ya $3.55 billion, ongezeko la 12% la thamani kutoka msimu uliopita.
Barcelona
huenda wakawapita wapinzani wao kutokana na mkataba wa $400 million la
utengenezaji upya uwanja wao wa Camp Nou, ambao unategemea kukamilika
ndani ya miaka mitano.
Timu
ya 3 kwa thamani kubwa ni Manchester United, klabu ambayo ipo kwenye
soko la hisa. Forbes wanaitaja kuwa na thamani ya $3.32billion, ongezeko
la asilimia 7 la thamani kutoka mwaka jana. Man United wametengeneza
faida ya $190m kwa msimu wa 2014-15, kwenye listi hii Man United ndio
timu iliyoingiza faida kubwa kwa upande wa soka lakini wapo nyuma ya
Dallas Cowboys ($270 million) na New England Patriots ($195 million)
kiujumla.

0 comments:
Post a Comment