Mabondia wa
Tanzania pamoja na mabondia kutoka nje ya Tanzania wamepima uzito kabla
ya mapambano ya masumbwi ya kimataifa yatakaofanyika Jumamosi uwanja wa
ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mabondia wa Tanzania
watakaopanda Ulingoni ni Thomas Mashali, Abdallah Pazi, Fransic
Miyeyusho, Lulu Kayage na Swalehe Mkalekwa.
Bondia Thomas Mashali 'Simba Asiyefugika' atakuwa anagombea ubingwa wa dunia mkanda wa U.B.O kilo 76 dhidi ya bondia Sajjad Mehrab kutoka Iran, Cosmas Cheka atakuwa akigombea ubingwa wa Dunia wa U.B.O uzito wa Unyoya kilo 59 dhidi ya Fransic Kimani kutoka kenya .



0 comments:
Post a Comment