Mashindano
ya Olimpiki ambayo hufanyika kila baada ya miaka minne yakihusisha
michezo tofautitofauti na ikiwa imesalia miezi mitatu kufanyika kwa
mashindano hayo huko mjini Rio de Jenairo Brazil msimu huu lakini
taarifa zinazoripotiwa ni kuwa msimu huu huenda yakaingia dosari baada
ya madaktari 150 Duniani pamoja na wataalamu wa maswala ya afya kuungana
pamoja kupinga mashindano kufanyika.

Madaktari
hao wametahadharisha juu ya usalama wa afya za wachezaji, waandishi wa
habari pamoja na wote watakaohusika katika mashindano hayo.
Wamependekeza mashindano hayo yaahirishwe kwa sasa mpaka kutakapokuwa na
usalama wa kiafya nchini humo au yafanyike sehemu nyingine tofauti na
Brazil. Sababu kuu ni kutokana na uwepo wa virusi vya zika nchini
Brazil wakihofia kuendelea kusambaa kwa virusi hivyo.

Virusi vya Zika uambukizwa kwa kung’atwa na mbu aina ya Aedes aegypti ambaye pia usambaza homa za dengue pamoja na homa ya manjano ambapo muathirika wa virusi vya zika hujifungua
mtoto mwenye kichwa kidogo kupita kiasi hali hiyo ikiambatana na
maumivu makali ya kichwa, ngozi kusinyaa, misuli kukaza pamoja na homa
za mara kwa mara.

0 comments:
Post a Comment