Mabondia wa
ngumi za kulipwa Mtanzania, Thomas Mshali ‘Simba asiyefugika’ na
Muiran, Sajjad Mehrabi wametambiana kupasuana kesho Jumamosi katika
pambano la kugombania Ubingwa wa Dunia UBO linalotarajia kupigwa kwenye
Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar.
Sajjad
ambaye ni mara yake ya pili kuja baada ya mwaka 2014 kucheza pambano
lisilo kuwa la ubingwa dhidi ya Francis Cheka ambalo lilimalizika kwa
sare kabla ya safari hii kurejea tena nchini kwa ajili ya kuchueza
dhidi ya Mashali.
Mabondia
hao kila mmoja ameonyesha nia ya kutaka kuibuka na ubingwa wa pambano
hilo litakalo kuwa la raundi 12 kwa kutamkiana maneno ya vitisho vya
kutaka kutoana roho ulingoni.
Mashali
alisema hatarajii kuwaangusha Watanzania kesho kwa kuhakikisha anampa
kichapo kikali mpinzani wake na ikiwezekana kumtoa roho ulingoni .
“Maandalizi
makali niliyofanya nina uhakika yule Mwarabu hachomoki, yaani nife mimi
au yeye lakini na kuhakikishia ubingwa utabaki Tanzania kwa sababu
hapa achezi Mashali hapa inacheza Tanzania hivyo nitapambana kwa ajili
ya Watanzania tu si zaidi ya hapo kwani lengo langu nataka akaisimulie
kwao kuwa Mashali ni nani”.
Kwa
upande wa Muiran, alisema kuwa: “Sioni sababu ya kushindwa kumchapa
mpinzani wangu maana bado hayupo sawa kabisa mpaka aweze kunipiga mimi
kwa sababu nimekuja tena hapa kwa ajili ya kuondoka na ushindi na siyo
jambo lengine kwani raundi ndiyo zitaonyesha nani anastahili kuitwa
bingwa”.
Licha
ya pambano hilo mabondia wengine watakaopanda ulingoni ni Francis
Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ dhidi ya Frank Kiwarabi, Saleh Mkalekwa dhidi ya
Joseph Onyango, wakati Ramadhani Shauri, Lulu Kayage na Nassibu
Ramadhan hao watacheza na mabondia kutoka katika nchini Kenya, Malawi na
Uganda.

0 comments:
Post a Comment