MECHI YA MAN UNITED V BOURNEMOUTH YAFUTWA, SABABU ZA KIUSALAMA!


OLDTRAFFORD-ABANDONED
MECHI ya BPL, Ligi Kuu England, kati ya Manchester United na Bournemouth iliyokuwa ichezwe Uwanjani Old Trafford imefutwa kwa sababu za kiusalama.

Mechi ni ya mwisho ya Ligi kwa Timu hizo mbili na imefutwa baada ya kugundulika kwa mzigo wa mashaka kwenye Jukwaa la Stetford End na kuwafanya Walinzi kuwatoa nje ya Uwanja Mashabiki waliokuwa Jukwaani hapo pamoja na wale wa Jukwaa la Sir Alex Ferguson huku Polisi na Mbwa spesho wa Polisi wakipita kila sehemu kuchunguza.

Baada ya muda mfupi Washabiki wakatangaziwa kuwa Mechi hiyo imefutwa na haijajulikana lini itachezwa.
Man United walikuwa wanahitaji kushinda Mechi hii na Man Cuty kufungwa hii leo ili waipiku Man City katika Nafasi ya 4 ili wacheze UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Hadi Mapumziko City wakicheza Ugenini huko Liberty Stadium walikuwa Sare 1-1 na Swansea City.
LIGI KUU ENGLAND

Jumapili Mei 15

Mechi za Mwisho za Ligi, zote kuanza Saa 11 Jioni

MATOKEI HADI HAFTAIMU

Arsenal  1 Aston Villa 0     
Chelsea 0 Leicester 0       
Everton 3 Norwich 0         
Man United v Bournemouth (IMEFUTWA)              
Newcastle 2 Tottenham 0             
Southampton 1 Crystal Palace 0              
Stoke v West Ham            
Swansea 1 Man City 1      
Watford 1 Sunderland 2             
West Brom 1 Liverpool 1
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment