
AC Milan imeadhimisha miaka 26 tangu ilipofanikiwa kutetea kombe la mabingwa Ulaya wakati huo likiitwa European Cup. AC Milan ilitetea taji hilo mwaka 1990, Franco Baresi anakumbuka mafanikio waliyofikia yeye na wakongwe wenzake waliokuwa kwenye kikosi cha Milan wakati huo.
Miongoni mwa sura za ma-striker wa zamani walioonekana kwenye UEFA Champions Gallery mjini Milan baada ya kufunguliwa kwa rasmi kwa sherehe hizo ni mkongwe Franco Baresi ambaye alikuwa amebeba picha yake inayomwonesha akiwa amenyanyua ndoo ya ubingwa wa klabu bingwa Ulaya enzi hizo kwenye usiku wa Vienna.
Ilikuwa ni May 23, 1990 wakati AC Milan ilipofanikiwa kutetea taji lao kwa kuifunga Benfica kwa bao 1-0. Tangu kipindi hicho, miamba hiyo ya soka la Italia haijafanikiwa kuifikia rekodi hiyo ikiwa imeshapita miaka 26 sasa tangu kuwekwa kwa rekodi hiyo.
Akiwa kama nahodha siku hiyo, Baresi anaungana na orodha ya ma-star wengine wa mashindano hayo kuelezea picha hizo zinawakumbusha nini leo, ikiwa ni sehemu ya ku- promote UEFA Champions Gallery ambayo imefunguliwa kuanzia jana na itafungwa siku ya Jumapili May 29.

0 comments:
Post a Comment