Baada ya kupata sifa nzuri katika kusimamia usajili mzuri kwa bei nzuri katika klabu ya Sevilla, mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ‘Director Monchi’ameripotiwa yupo mbioni kuachana na klabu hiyo.
Monchi aka Mr Moneyball ameripotiwa anaondoka Sevilla na huenda akaenda kumsaidia kazi Jose Mourinho pale Man United au Zinedine Zidane @SantiagoBernabeu.Kuondoka kwa Monchi litakuwa ni pigo kubwa kwa Sevilla, ambao wamekuwa wakimtegemea sana katika masuala ya usajili -akidili na kuimarisha kikosi kinapodhoofika – Monchi hutengeneza mazingira ya kibiashara yanayoitengenezea klabu faida kubwa.
Chini ya uongozi wake, Sevilla wamefanikiwa kushinda makombe 9, yakiwemo matano ya Europa League.
Sababu binafsi ndio zinaaminila kuwa chanzo cha kuondoka kwa Monchi, na uhamisho wa kwenda aidha Real Madrid au Manchester United.
Hata hivyo, Monchi ameripotiwa anahitaji kuondoka nje ya La Liga, na hivyo huenda mkurugenzi huyo mwenye umri wa miaka 47 akaitosa Madrid kisha kujiunga na Jose Mourinho.

0 comments:
Post a Comment