NENO LA KWANZA LA XHAKA BAADA YA KUSAINI MKATABA ARSENAL

Grant
Grant
Arsenal tayari wamethibitisha kumsajili kiungo wa Borussia Monchengladbach Granit Xhaka kwa ada inayokadiriwa kufuka paundi milioni 30.
Mswizi huyo atakuwepo katika michuano ya EURO 2016 huko nchini Ufaransa na atajiunga na Arsenal punde tu baada ya michuano hiyo kumalizika.
“Ninajivunia sana kujiunga na Arsenal,” alisema Xhaka. “Ninasubiri kwa hamu sana kuungana na wenzangu kuiwakilisha timu yetu katika michuano mbalimbali hasa ligi kuu. Ninajitoa kwa kila hali kuhakikisha kuwa naipa makombe Arsenal na kuwafanya mashabiki kuwa na furaha.”
Kwa upande wake kocha Arsene Wenger amesema: “Granit Xhaka ni mchezaji kijana na mwenye uwezo wa hali ya juu, na kitu kizuri zaidi tayari ana uzoefu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na ligi ya Bundesliga.
“Tumekuwa tukimwangalia kwa muda mrefu sana kwa hiyo ni mchezaji ambaye tunatarajia ataongeza ubora katika kikosi chetu. Tunamtakia Granit kila la heri katika Euro 2016 akiwa na taifa lake la Uswizi na tunamngoja kwa hamu kuungana na wenzake pindi michuano hiyo itakapomalizika kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment