Straika
wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma, amesema wazi kuwa haifahamu sana TP
Mazembe ya DR Congo lakini atakapokutana nayo atahakikisha anaifunga.
Hiyo
imekuja baada ya Yanga kupangiwa TP Mazembe kama moja ya timu zilizopo
kwenye kundi lao la Kombe la Shirikisho Afrika, timu nyingine ni Medeama
ya Ghana na MO Bejaia ya Algeria.
Ngoma
amefunguka kuwa kilichobaki sasa ni kupambana na siyo kuangalia
wanawafahamu vipi wapinzani wao, hivyo hata kama hawajui, hiyo haiwezi
kuzuia wao kupigania matokeo yaliyo bora kwao kwa ajili ya kuzidi
kusonga mbele.
“Siwafahamu
Mazembe kwa kiasi kikubwa lakini shida yetu ni kupata matokeo mazuri
yenye faida kwetu, tutapambana na lengo letu ni ushindi tu, kuwafunga
itakuwa matokeo mazuri zaidi kwetu, kwa hiyo kilichopo ni kutafuta
ushindi tu,” alisema Ngoma aliyeifungia Yanga mabao 17 kwenye Ligi Kuu
Bara msimu uliopita.
Yanga
inatarajia kuikaribisha Mazembe kati ya Juni 28 au 29 katika mchezo wa
nyumbani kabla ya kurudiana huko DR Congo kati ya Agosti 23 au 24, mwaka
huu.


0 comments:
Post a Comment