Pamoja na kujiuzulu Stars – Mkwasa amuita Cannavaro kuziba pengo la Yondani

img_7958-1.jpg
img_7958-1.jpgPamoja na kutangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania, kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Boniface Mkwasa leo ametaja kikosi chenye majina ya wachezaji 27 kitakachoingia kambini kujiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya pamoja na ile ya kufuzu kwa ajili ya fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri na kujumuisha jina la nahodha wa zamani aliyejiuzulu Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Cannavaro ameitwa kuziba pengo la Kelvin Yondani ambaye anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano na hivyo kuikosa mechi ya Misri Juni 4.
Kikosi cha Taifa Stars kitaingia kambini tarehe 23 kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kenya utakaochezwa tarehe 29 Mei jijini Nairobi.
Baada ya hapo Taifa Stars itarejea Dar kukamilisha maandalizi ya kuivaa Misri katika mchezo ambao inahitaji ushindi wa angalau mabao matatu kuweka hai matumaini ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon mwakani.
Kikosi kamili cha Stars: 
Walinda Milango: Deo Munish (Yanga), Aishi Manula (Azam) Benno Kakolanya (Prisons).
Walinzi: Juma Abdul, Haji Mwinyi, Nadir Haroub (Yanga), Erasto Nyoni, David Mwantika, Aggrey Morris (Azam), Mohamed Tshabalala (Simba), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar).
Viungo: Himid Mao, Farid Mussa (Azam), Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto (Simba), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar),Hassan Kabunda (Mwadui), Juma Mahadhi (Coastal Union), Ismail Issa Juma (JKU).
Washambuliaji: Elias Maguri (Stand United), John Bocco (Azam) Ibrahim Hajib (Simba), Mbwana Samatta (Genk GRC, Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe)
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment