PATASHIKA KUCHANIKA KESHO HARAMBEE STAR VS TAIFA STAR

    Timu ya Taifa ya Tanzania inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa Kenya Mei 29, jijini Nairobi.
Mchezo huo utachezwa jijini Nairobi Mei, 29 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote mbili kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika mwezi Juni, 2016 ambapo Taifa Stars itacheza dhidi ya Misri Juni 04, mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
TFF kwa kushirkiana na FKF zimekubaliana kuwepo kwa mchezo huo wa kirafiki, utakotumika kama sehemu za maandalizi kwa timu zote kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 mwezi Juni.
Kikosi cha Taifa Stars kinachonolewa na kocha mkuu, Charles Boniface Mkwasa kinatarajiwa kuingia kambini mwezi Mei, mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Vodacom (VPL) kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuwakabili Misri mwezi Juni, 2016.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment