Vikundi
sita kati ya 12 vilivyoshiriki mashindano ya Ngoma za Asili katika
Tamasha la Majimaji Selebuka linaloendelea mjini Songea, vimejikita
kusifia utawala wa awamu ya tano chini ya Dk John Pombe Magufuli, kama
chambo ya kujinyakulia ushindi nafasi ya kwanza.
![]() |
| RAIS MAGUFULI |
Tamasha
hilo linaloendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya
Majimaji mjini Songea, jana liliingia katika siku ya pili ambapo jana
ilikuwa ni zamu ya mashindano ya ngoma za asili ambazo mshindi
anatarajiwa kupatikana leo Jumatatu.
Vikundi
vya Boma Jaribu, Mganda Kilagano, Matogolo, Kioda Mji Mwema, Mganda
Mshindo na Boma Kilagano vilijikuta vikigonganisha nyimbo, zote zenye
ujumbe wa kusifu uongozi wa Dk Magufuli kwa jinsi anavyokula sahani moja
na mafisadi, watumishi hewa na kutetea haki za wanyonge.
Mashindano
hayo yaligawanywa katika vipengele vitatu; Ngoma ya Kioda, Ngoma ya
Mganda na Mchanganyiko. Mshindi kwa kila kipengele atajinyakulia laki
tatu, laki mbili kwa mshindi wa pili na laki moja kwa mshindi wa tatu.


0 comments:
Post a Comment