Ranieri: Klabu tajiri kutawala ligi ya Uingereza

Image copyrightGetty
Image captionClaudio Ranieri
Klabu tajiri katika ligi kuu ya Uingereza zitatawala kwa miongo miwili ijayo licha ya kufuatia ushindi wa klabu ya Leicester kulingana na mkufunzi Claudio Ranieri.
Kikosi cha Leicester kiligharimu pauni milioni 57, kikiwa ndicho cha bei ya chini zaidi miongoni mwa timu zilizopo katika nusu ya kwanza ya jedwali la ligi hiyo.
Fedha nyingi hujenga timu kubwa na kama kawaida timu kubwa hushinda.
Sasa tunaweza kusema ni asilimia 99, alisema Ranieri.
Image copyrightGetty
Image captionMashabiki wa Leicester wakifurahia ushindi wa timu yao
Msimu ujao itakuwa hali kama hiyo na miaka 10 ama 20 ijayo, hali itakuwa kama kawaida kwamba timu kubwa ndizo zitakazoshinda, alisema meneja wa Leicester.
Ranieri alisema kwamba ushindi kama wa timu yake hutokea mara moja katika kipindi cha miaka 20 akitoa mfano wa Nottignham Forest mwaka 1978 na Blackburn Rovers 1995.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment