
Sir Bobby Charlton Jana alimpokea Meneja mpya wa Manchester United Jose Mourinho kwenye Kituo cha Mazoezi cha Klabu hiyo huko Carrington ambacho huitwa Aon Training Complex.

Charlton, Lejendari wa Man United ambae sasa ni mmoja wa Wakurugenzi wake, alimkaribisha Mourinho kwa kumpa hongera na kumwambia ‘nasikia furaha kukuona hapa’.
Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Mourinho, mwenye Miaka 53, kufika Carrington na aliambatana na Msaidizi wake wa Siku nyingi, Rui Faria, na kusindikizwa na Makamu Mwenyekiti Mtendaji Ed Woodward.

Mourinho, ambae aliwahi kuwa Meneja wa FC Porto, Chelsea, Inter Milan na Real Madrid, aliteuliwa kuwa Meneja mpya wa Man United kumrithi Louis van Gaal Ijumaa iliyopita.

Mourinho anatarajiwa kuanza rasmi kuanza kazi na Kikosi cha Wachezaji ambao hawatashiriki Fainali za EURO 2016 na Copa America na ambao watarudi toka Likizo na kujumuika kwa Mazoezi kwa ajili ya Msimu mpya hapo Julai 4.

RASHFORD ASAINI DILI MPYA

Marcus Rashford amesaini Mkataba mpya na Manchester United ambao utamweka Klabuni hapo hadi 2020 huku kukiwa na Kipengele cha kubakia kwa Mwaka Mmoja zaidi ya hapo.
Rashford, mwenye Miaka 18, amekulia Man United akianzia kwenye Chuo cha Soka Klabuni hapo na alipewa fursa kuichezea Timu ya Kwanza ya Man United kwa mara ya kwanza Msimu huu kwenye Mechi ya EUROPA LIGI dhidi ya FC Midtjylland na kupiga Bao 2 na Siku 3 baadae akacheza tena Mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal na kupiga tena Bao 2.
Msimu huu, uliokwisha Mei 21, Rashord aliichezea Man United Mechi 17 na kufunga Bao 8.
Akiongea baada ya kusaini wa Mkataba, Makamu Mwenyekiti Mtendaji Ed Woodward alisema:
"Marcus ni Mchezaji mwenye kipaji cha asili. Ametumia fursa yake vizuri na amejumuika vizuri na Timu ya Kwanza. Nimefurahi amesaini Mkataba na yupo kwenye Klabu sahihi kwa maendeleo yake. Bado ni Kijana mdogo mno na anapaswa kuwa mvumilivu lakini anaendelea vizuri na tuna matumaini atafanikiwa vyema.”
Nae Marcus Rashford amesema: “Nimefurahishwa mno kusaini Mkataba mpya. Daima nimekuwa shabiki wa Manchester United na kuichezea Timu ya Kwanza ni ndoto iliyokuwa kweli. Nashukuru mno kwa fursa ya kuhakikisha uwezo wangu. Kuichezea Klabu kubwa kabisa Duniani ina maana kubwa sana kwangu na Familia yangu!”
BORTHWICK-JACKSON ASAINI DILI MPYA
Cameron Borthwick-Jackson amesaini Mkataba mpya na Manchester United ambao utamweka Klabuni hapo hadi 2020 huku kukiwa na Kipengele cha kubakia kwa Mwaka Mmoja zaidi ya hapo.
Borthwick-Jackson, mwenye Miaka 19, amekulia hapo Man United kutokea Chuo cha Soka na kuichezea Timu ya Kwanza kwa mara ya kwanza kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Mwezi Novemba dhidi ya West Bromwich Albion.
Msimu huu, Cameron amecheza Mechi 14 na pia kushinda Tuzo ya Mchezaji bora wa Mwaka kwa Vijana chini ya Miaka 21.
CARRICK KUBAKIA MAN UNITED
Michael Carrick amepewa nyongeza ya Mkataba wa Mwaka Mmoja na Meneja mpya Jose Mourinho na hivi sasa Mchezaji huyo anatafakari Ofa hiyo.
Carrick, mwenye Miaka 34 aliejiunga na Man united Mwaka 2006 akitokea Tottenham, anamaliza Mkataba wake wa sasa na Man United mwishoni mwa Juni.
Lakini kutua kwa Mourinho kumemhakikishia atabakia Old Trafford kwa Msimu Mmoja zaidi.

0 comments:
Post a Comment