Zikiwa
zimebaki siku 14 tu kabla ya tamasha la kila mwaka la Majimaji Selebuka
2016 kuanza Mei 28, mwaka huu mjini Songea, waratibu wa tamasha hilo
bado wanasaka udhamini kwa ajili ya kufanikisha lengo lao.
Tamasha
hilo linaloratibiwa na Asasi ya Songea & Mississippi (Somi)
litachukua muda wa wiki nzima katika Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa
Vita vya Majimaji uliopo Songea Mjini ambapo zinahitajika Sh milioni 45
ili lifanyike kikamilifu.
Mratibu
wa tamasha hilo, Reinafrida Rwezaura ameliambia Championi Jumamosi
kuwa, lengo la tamasha hilo ni kuinua vipaji, kutangaza utalii wa Mkoa
wa Ruvuma pamoja na kumuinua mwananchi wa chini kupitia maonyesho na
mafunzo ya ujasiriamali yatakayokuwepo.
Pia
kutakuwa na mashindano ya riadha, mbio za baiskeli ambapo kutakuwa na
washiriki kutoka mataifa mbalimbali, ‘debate’ kwa shule za sekondari,
utalii wa ndani na ngoma za asili.
“Kwa
niaba ya asasi nipongeze kampuni zilizojitokeza kutusapoti mpaka sasa,
lakini bado tunahitaji udhamini zaidi ili kutimiza azma yetu. Tunaomba
kampuni na watu binafsi kutusapoti,” alisema Rwezaura.
Mpaka sasa tamasha hilo limefanikiwa kupigwa jeki na Kampuni ya Bakhresa, Global Publishers, CRDB, Chuo Kikuu Huri

0 comments:
Post a Comment