
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Nusu Fainali
Mechi za Pili
**Saa 3 Dakika 45 Usiku
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
Jumanne Mei 3
Bayern Munich v Atletico Madrid [0-1]
Jumatano Mei 4
Real Madrid v Manchester City [0-0]
VIGOGO wa Germany Bayern Munich Jumanne Usiku wanatinga Uwanjani kwao Allianza Arena kurudiana na Atletico Madrid ya Spain katika Mechi ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huku wakitakiwa kupindua kipigo cha Bao 1-0 ili wao watinge Fainali.
Wiki iliyopita huko Vicente Calderon Jijini Madrid na Bao la Dakika ya 11 la
Niguez liliwapa Atletico ushindi wa 1-0.
Bayern wanatinga kwenye Mechi hii muhimu wakiwa na Majeruhi kadhaa ambao ni Holger Badstuber, Arjen Robben na Franck Ribery ambae huenda akarejea.
Atletico wao hawana Wachezaji majeruhi.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Bayern Munich: Neuer; Lahm, Boateng, Martinez, Alaba; Muller, Vidal, Thiago; Costa, Lewandowski, Ribery
Atletico Madrid: Oblak; Juanfran, Godin, Gimenez, Luis; Saul, Gabi, Fernandez, Koke; F Torres, Griezmann
REFA: Cüneyt Çakır (Turkey)
Fainali
Jumamosi Mei 28
**Saa 3 Dakika 45 Usiku

0 comments:
Post a Comment