![]() |
| ULIMBOKA (KULIA) |
Baada
ya Simba kukosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa nne mfululizo,
mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Ulimboka Mwakingwe, amesema hali
hiyo inatokana na viongozi wa klabu hiyo kufanya usajili mbovu kila
msimu.
Mara ya mwisho Simba kuchukua ubingwa wa ligi kuu ilikuwa ni msimu wa 2011/2012.
“Kiukweli
Simba inakosea katika sehemu tatu, mojawapo ni katika suala zima la
usajili kwa sababu kamati inayohusika na ishu hiyo, wengi wao hawajui
mpira, hilo ni tatizo na ni ngumu kuweza kupata wachezaji wazuri.
“Unajua
Simba lazima itafute watu ambao wanauelewa mpira vizuri kwa maana ya
kuucheza, wawape kazi hiyo kwa sababu wanajua vizuri wachezaji wa aina
gani watakaoweza kuisaidia Simba,” alisema Ulimboka.
Ulimboka
alikuwa kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha Simba kilichofuzu
kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa wakati huo ni Klabu Bingwa
Afrika, mwaka 2003.
Simba
ilivuka kwenda hatua hiyo kwa kuwang'oa Zamalek wakati huo wakiwa
mabingwa watetezi Afrika na timu bora kwa upande wa klabu barani Afrika


0 comments:
Post a Comment