
Chelsea na Tottenham zimefunguliwa Mashitaka Matatu na FA, Chama cha Soka England, kwa kushindwa kudhibiti Wachezaji wao wakati wa Mechi yao ya Jumatatu Usiku ya Ligi Kuu England Uwanjani Stamford Bridge.
Pamoja na Klabu hizo, Kiungo wa Spurs, Mousa Dembele, mwenye Miaka 28, nae ameshitakiwa kwa Kosa la kufanya vurugu kupindukia na, kama ilivyodokezwa na FA, Kosa lake ni kubwa na yupo hatarini kufungiwa zaidi ya zile Mechi 3 za kawaida ikiwa atapatikana na hatia.

Dembele anadaiwa kumtia Kidole machoni Straika wa Chelsea Diego Costa na amepewa hadi Alhamisi Jioni kujibu Shitaka lake.
Klabu za Chelsea na Spurs zimepewa hadi Jumatatu kujibu Mashitaka yao Matatu ya kuvunja Sheria ya FA E20 ya kudhibiti Wachezaji pamoja na Maafisa wao.
Mashitaka hayo Matatu yametokana na Matukio Matatu kwenye Mechi hiyo ya Dakika za 45 na 87 na pia mwishoni mwa Gemu hiyo ambayo Wanahabari huko Rngland wameibatiza ‘VITA YA DARAJANI.’
Katika Mechi hiyo, Chelsea walitoka nyuma 2-0 na kupata Sare ya 2-2 iliyofuta matumaini ya Ubingwa kwa Spurs na kuwapa Ubingwa wao wa kwanza Leicester City ambao wana Mechi 2 mkononi.
Vile vile kwenye Mechi hiyo, Kadi za Njano 12 zilitolewa, 9 kwa Spurs waliovunja Rekodi ya Kadi nyingine katika Mechi moja ya Ligi Kuu England.


0 comments:
Post a Comment