WAKONGWE WA AC MILAN NA INTER MILAN WAZINDUA SHEREHE ZA FAINALI YA UEFA

UEFA-Legends
UEFA-Legends
UEFA Champions League Gallery tayari imeshafunguliwa, shereheza za kusherekea zaidi ya miongo sita ya michuano ya vilabu bingwa Ulaya zinaendelea mjini Milan, huku ma-legend wanne kutoka miamba ya soka ya jiji la Milan wakipata fursa ya kuzindua sherehe hizo.
Wakongwe wa AC Milan na Inter Milan walijumuika pamoja kwenye ufunguzi wa UEFA Champions Gallery, ambayo itakuwa ni kivutio kwenye sherehe za UEFA Champions League mjini Milan hadi kufikia siku ya Jumapili May 29.
Massimo Ambrosini, Ivan Córdoba, Cafu na Dejan Stanković walikuwa wakikumbuka enzi zao pamoja kundi kubwa la wadau wa soka mjini Milan pamoja na vyombo vya habari, sherehe hizo zimeongozwa na mwandishi maarufu Gabriele Marcotti huku mkurugenzi wa mashindano kutoka UEFA Giorgio Marchetti akitoa ujumbe wa mashindano katika msimu huu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment