YANGA: UWEZO TUNAO, NGUVU TUNAZO, SABABU TUNAZO NA NIA TUNAYO YA KUMSAJILI TCHETCHE


Kutoka kushoto: Vicent Bosou, Kipre Tchetche na Pascal Wawa wakipiga story mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya FA Cup kati ya Azam FC dhidi ya Yanga juma lililopita
Kutoka kushoto: Vicent Bosou, Kipre Tchetche na Pascal Wawa wakipiga story mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya FA Cup kati ya Azam FC dhidi ya Yanga juma lililopita
Kunatetesi nyingi kwamba huenda mshambuliaji wa Azam FC Kipre Tchetche akajiunga na Yanga kutokana na mkataba wa nyota huyo kuwa unaelekea ukingoni ndani ya klabu ya Azam.
Ofisa habari wa klabu ya Yanga amesema timu yao inatamani pia huduma ya raia huyo wa Ivory Coast ambaye anafanya vizuri kwenye michuano ya ndani na ile ya kimataifa.
“Ni mchezaji wa aina yake ambaye hata sisi Yanga tunatamani kuwanaye. Mimi niseme tu, wana Yanga wasiwe na wasiwasi kama wanamtaka Kipre Tchetche watuambie sisi tutavunja makabati, nguvu tunazo, uwezo tunao, nia tunayo na sababu tunayo kwasababu tunamtaka mcheaji kwa ajili ya mashindano ya kimataifa”.
“Secretariat ya Yanga inasubiri ripoti ya technical benchi lakini pia tunasubiri mapendekezo ya kamati tendaji pamoja na kamati ya mashindano ili sisi tuweze kufanyia kazi yale ambayo yamependekezwa na mwalimu pamoja na benchi la ufundi na kamati ya utendaji ili yakija kwetu sisi tunafanya utekelezaji”, anasema  Jerry Muro ofisa habari wa Yanga.
“Tchetche ameifungia Yanga jumla ya magoli 12 kwenye msimu wa VPL uliomalizika hivi karibuni lakini nyota huyo amekuwa akiandamwa na majeruhi ya hapa na pale ambayo yamesababisha akose mechi kadhaa za ligi pamoja na za mashindano ya kimataifa”.
Hivi karibuni uongozi wa Azam FC ulikaririwa ukisema, klabu yao inataka kuwekeza nguvu nyingi katika kukuza na kulea vijana ili baadaye waisaidie klabu yao pamoja na kuwauza nje ya nchi ili kupunguza matumizi ya pesa nyingi katika usajili wa wachezaji wa nje ikiwa ni pamoja na kuwalipa mishahara mikubwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment