Muzamil anakuwa mchezaji wa tatu kusaini Simba, baada ya beki Emmanuel Semwanza na kiungo Jamal Mnyate wote kutoka Mwadui ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amekataa kutaja wachezaji waliosajiliwa hadi sasa, kwa madai kuwa watatangaza rasmi kesho, lakini BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE inafahamu Semwanza, Mnyate na Muzamil ndiyo wamesaini kati ya sita wanaowataka.
![]() |
| Muzamil Yassin akimiliki mpira mbele ya Peter Mwalyanzi wa Simba |
Wengine ambao Simba ilikuwa inahaha kukamilisha usajili wao jana ni winga machachari wa Mtibwa Sugar, Shizza Ramadhani Kichuya, Salim Kimenya na Jeremiah Juma wa Prisons.
“Siwezi kukuambia tumemsajili nani na nani, ila nataka nikuhakikishie tumekwishapata saini sita za askari shupavu, weledi na waaminifu, watakaorejesha heshima ya Mnyama msimu ujao,”alisema Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Alipoulizwa kama saini hizo ni za wachezaji wa nyumbani tu au na wa kigeni pia, Hans Poppe alisema; “Mtajua kesho.


0 comments:
Post a Comment