
Ni wazi sasa kiungo wa Yanga Salum Telela hatokuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa ajili ya msimu ujao baada ya nyota huyo kumaliza mkataba wake wa kuitumikia klabu hiyo na uongozi wa Yanga haujamwongezea mkataba mpya hadi sasa.
Beki namba wa kulia wa Yanga Juma Abdul Juma Abdul ni miongoni mwa marafiki wa karibu wa Telela, kwa mujibu wa Naipenda Yanga facebook page Juma Abdul jana aliandika ujumbe kupitia account yake ya Instagram akitoa hisia zake juu ya rafikiyake kutemwa Yanga.
“Hakika safari ya maisha kwa sisi wanadamu tunapitia vikwazo vingi sana, NEVER GIVE UP..Abo Master kwani umpigapo teke chura ndipo umuongezeapo hatua mbili mbele, kwani sisi sote Mungu wetu ni mmoja na ipo siku itafahamika mbivu na mbichi.”
Ni maneno ya Juma Abdul kupitia akaunti yake ya Instagram akielezea hisia zake kwa rafiki yake Salum Telela waliyesoma pamoja Makongo pia wakicheza pamoja Yanga lakini hivi karibuni Yanga hawajamuongeza mkataba.
Telela ni miongoni mwa wachezaji waliodumu Yanga kwa muda mrefu, nahodha huyo wa zamani wa Moro United alitua Yanga mwaka 2010 hadi sasa akiwa ameitumikia Yanga kwa misimu 6.
Chanzo: Naipenda Yanga facebook (page https://www.facebook.com/YangaDaima/)

0 comments:
Post a Comment